Mutua akosoa uamuzi wa mahakama kuhusu BBI

0

Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua amekosoa uamuzi wa mahakama uliosimamia marekebisho ya katiba kupitia BBI.

Kiongozi huyo wa chama cha Maendeleo Chap Chap amesema iwapo majaji wa mahakama kuu wangekuwa na ufahamu kuhusu maswala yanayoangazia uongozi na uchumi wa taifa hili,hawangesimamisha mchakato wa kubadilisha katiba.

Kwa mujibu wa Mutua, kuna umuhimu mkubwa kwa umma iwapo BBI itapitishwa badala ya kusimamishwa walivyofanya majaji wa mahakama kuu.

Miongoni mwa mapendekezo ambayo gavana Mutua anasema yatakuwa na umuhimu kwa Wakenya ni pamoja na afueni ya kutolipa ushuru kwa biashara ndogo ndogo pamoja na kutenga rasilimali zaidi kwa serikali za kaunti ili kuboresha ugatuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here