Mshukiwa wa mauaji ya familia yake Kiambu hana akili timamu kushtakiwa

0

Lawrence Warunge anayetuhumiwa kuua watu wanne wa familia yake na mfanyikazi kaunti ya Kiambu hayuko sawa kiakili kujibu mashtaka dhidi yake.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa kiakili iliyowasilishwa mahakamani ambayo imeashiria kuwa mshukiwa hana akili timamu.

Warunge ataendelea kuzuiliwa huku akipokea matibabu hadi tarehe mosi Machi mwaka huu wakati kesi hiyo itatajwa.

Hakimu Patricia Gichohi amemuachiliwa huru mpenziwe Warunge Sarah Muthoni baada ya upande wa mashtaka kusema unalenga kumtumia kama shahidi kwenye kesi hiyo.

Warunge anatuhumiwa kutumia kisu kumuua babake Nicholas Njenga, mamake Annie Njenga, watoto wao Maxwell na Christian na mfanyikazi James Kinyanjui.

Warunge katika taraifa ya Polisi alikiri kupanga mauaji hayo ya kinyama kwa muda wa miezi mitatu na kisha kuyatekeleza.

Aliwaambia Polisi kwamba alisukumwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na kutizama filamu moja.

Aliongeza kwamba alikuwa amepanga kuiangamiza familia yake yote wawekimo dada zake wawili walioponea kwa sababu walikuwa wameenda shuleni ila njama yake ilitibuka waliporejea shuleni Januari 5 siku anayodaiwa kutekeleza mauaji hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here