Mbunge wa Likoni Mishi Mboko analitaka bunge kuidhinisha hoja inayoishinikiza serikali kuongeza muda wa mpango wa Kazi Mtaani uliozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta.
Mboko kwenye hoja hiyo anasema mpango huo ulikuwa umezisaidia familia nyingi kufuatia kutokea kwa janga la COVID19 na kuwaacha wengi bila kuwa na namna ya kutafuta shilingi.
Mbunge huyo anataka mpango huo kupelekwa katika kaunti zote 47 ili kushughulikia tatizo la ukosefu wa kazi miongoni mwa vijana na pia kuongeza malipo wanayopewa.
Awamu ya kwanza ya Kazi Mtaani ilianza Aprili mwaka jana katika kaunti 8 pekee ambapo vijana 26,000 waliajiriwa.
Awamu ya pili ilianza Julai mwaka jana katika kaunti 34 na kuwaajiri vijana 200,000.









