Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i ameondoa kafyuu ya siku thelathini ya kutotoka nje kuanzia saa kumi na mbili za jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi huko Kapedo kuzuia visa vya utovu wa usalama kwenye mpaka wa Baringo-Turkana.
Matiang’i katika taarifa amesema ingawaje hali ya utulivu imerejea katika maeneo hayo tangu kuwekwa kwa marufuku hiyo, maafisa wa usalama wataendelea kushirika doria akionya kwamba serikali haitasita kurejesha kafyuu hiyo iwapo hali itakuwa mbaya tena.
Hata hivyo, Matiang’i amesema vizuizi vya Polisi ndani ya Kapedo vitasalia huku maafisa wa usalama wakishiriki pakubwa katika kupeleka misaada ya kibinadamu kwa walioathirika.
Matiang’i ameongeza kuwa silaha haramu 53 zilisalimishwa kwa kundi lililokuwa linaongoza oparesheni ya usalama katika maeneo hayo.