Mkewe rais Bi. Margaret Kenyatta amepongeza kazi wanaoifanya wauguzi kuhakikisha kwamba umma umepata huduma za afya kwa haraka.
Kimsingi, mkewe rais amesifia kujitolea kwa wauguzi kuwasaidia akina mama kujifungua na kuwahudumia watoto kipindi hiki kigumu cha corona.
Bi. Kenyatta amezingatia kujitolea kwake kupitia kampeini ya Beyond Zero kuchangia katika kuimarisha sekta ya afya nchini.
Amesema ndio maana mchango wa wauguzi utapewa kipau mbele kwenye kongamano la Beyond Zero baadaye mwezi Septemba mwaka huu.