Mahojiano ya kuwatafuta makamishna wa IEBC yaendelea kwa siku ya 10

0

Mahojiano ya kuwatafuta makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka yameingia siku yake ya kumi huku watu watatu wakihojiwa.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kutoa zabuni katika tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Sellestine Kiuluku amekuwa na wakati mgumu kuelezea ni vipi utaratibu wa kisheria haukufuatwa wakati wa kununua vifaa vya uchaguzi kati ya mwaka 2010-2017.

Kiuluku ambaye pia alikuwa kamishna wa tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma SRC amejitenga na ukiukaji huo wa sheria na badala yake kusema kuwa hakuidhinisha zabuni yoyote ya vifaa vya uchaguzi ambayo baadaye ilizua utata.

Mwingine aliyehojiwa ni kanali mstaafu Saeed Salim Saeed ambaye ametetea idara ya jeshi kuhusiana na tuhuma za kushawishika kuunga mkono serikali iliyo madarakani wakati wa uchaguzi.

Kwa upande wake Dr. Salim Ndemo amekuwa na wakati mgumu kujibu baadhi ya maswali yanayohusiana na uchaguzi ikiwemo vigezo vinavyohitajika kwa wawaniaji wa kiti cha Urais.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here