Mahakama yamkosoa Uhuru kwa kuunda wadhifa wa makatibu wasaidizi (CAS)

0

Mahakama kuu imetaja kama ukiukaji wa katiba hatua ya rais Uhuru Kenyatta kubuni nafasi za makatibu wakuu wasaidizi (CAS) katika wizara zote.

Katika uamuzi wake kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani na mwanaharakati Okiya Omtatah, jaji wa mahakama kuu Anthony Mrima ameamuru kuwa mawaziri walioteuliwa rais aliposhinda muhula wa pili waidhinishwe na bunge la kitaifa kuhudumu kwa muhula wa pili.

Mawaziri hao ni pamoja na Fred Matiang’i (Usalama), James Macharia (Uchukuzi), Joe Mucheru (ICT), Eugene Wamalwa (Ugatuzi), Charles Keter (Kawi), Raychelle Omamo (Mambo ya Nje), Adan Mohamed, (Afrika Mashariki), Sicily Kariuki (Maji), Najib Balala (Utalii) na Amina Mohamed (Michezo).

Aidha, jaji huyo ameamuru kuwa makatibu wakuu ambao hawakuorodheshwa, kuhojiwa au kuteuliwa kulingana na sheria wako afisini kinyume cha sheria.

Hata hivyo jaji huyo amezuia utekelezwaji wa uamuzi huo kwa sababau taifa bado linapambana na janga la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here