Madaktari Kisumu wahepa kupata chanjo ya corona

0

Wahudumu wa afya kaunti ya Kisumu wanasitasita kujitokeza kupata chanjo ya corona na hivyo kuchelewesha shughuli nzima ya kutoa chanjo hiyo.

Gavana wa kaunti hiyo Profesa Anyang Nyong’o amelalama kuwa ni wahudumu wa afya wapatao 2,191 waliopata chanjo hiyo kinyume na 7,500 waliokuwa wametarajiwa kuchanjwa kufikia sasa.

Na sasa Profesa Nyong’o ameiagiza idara ya afya katika kaunti hiyo kuendelea mbele na shughuli hiyo ya kutoa chanjo kuanzia Jumatatu ijayo kwa makundi mengine yaliyokuwa yapewe kipau mbele hata kama madaktari hawatakuwa wamemaliziwa.

Gavana huyo vile vile ametaka kutekelezwa kikamilifu kwa masharti yote ya usalama kuzuia msambao wa virusi vya corona ikiwemo kuwazika wafu saa sabini na mbili baada ya kufariki, wanaohudhuria mazishi wawe mia moja na kusiwe na chakula kwenye matanga.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here