Maandamano Kayole kufuatia mauaji ya raia

0

Hali ya vuta nikuvute imeshuhudiwa Kayole, Nairobi leo kufuatia maandamano ya wakaazi kulalamikia mauaji ya kijana mmoja anayedaiwa kuuawa na Polisi.

Wakaazi hao wanawatuhumu Polisi kwa kumuua jamaa huyo baada ya kumshika akiwa nje wakati wa kafyuu.

Inadaiwa John Kiiru alipatwa na polisi katika kituo cha Tushauriane akiwa kwa bodaboda kuelekea nyumbani baada ya saa nne usiku wakati polisi hao walimchapa hadi kufa.

Waandamanaji hao wamechoma magurudumu na kufunga barabara wakishinikiza haki kwa familia ya mwendazake.

Kisa hiki kinaongeza orodha ya visa vya polisi kudaiwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wananchi.

Mapema wiki hii maafisa sita walifikishwa mahakamani kwa madai ya kuua ndugu wawili waliokamatwa nje wakati wa kafyuu katika kaunti ya Embu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here