Kenya yawanyima kibali wanariadha wake kushiriki mbio za masafa marefu Tanzania

0

Serikali ya Kenya imekataa kuwaidhinisha wanariadha wake kushiriki mbio za masafa marefu za Kilimanjaro Marathon nchini Tanzania kwa kuhofia janga la corona.

Katika taarifa, Shirikisho la Riadha nchini limetoa wito kwa “wanariadha wote kutosafiri Tanzania kushiriki mashindano hayo”.

Mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF- yataandaliwa Jumapili hii chini ya mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika.

Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

Tanzania haijakuwa ikitoa data ya hali ya corona nchini humo tangu kati kati ya mwaka jana.

Mapema wiki hii Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa wito kwa Tanzania kuanza kutoa data ya watu walioambukizwa virusi vya corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here