Kenya yashinda dhahabu kwenye mbio za mita 800 mjini Tokyo, Japan

0

Hatimaye Kenya imeshinda medali ya DHAHABU ya kwanza kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea mjini Tokyo, Japan.

Emmanuel Korir aliishindia Kenya DHAHABU kwenye fainali ya mbio za Mita 800 kwa wanaume na kufuatiwa na mwenzake Ferguson Rotich aliyenyakua nishani ya FEDHA baada ya kumaliza wa pili.

Awali, Kenya ilishindwa kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi kwa wanawake.

Mwanariadha Peruth Chemutai wa Uganda ameshinda DHAHABU ya kwanza kwa taifa lake huku Mkenya Hyvin Kiyeng akishinda nishani ya SHABA baada ya kumaliza wa tatu.

Bingwa mtetezi katika mashindano hayo ya Olimpiki Faith Kipyegon alimaliza wa kwanza na kufuzu kwenye fainali za Mita 1,500 kwa wanawake.

Mwenzake Winnie Chebet alianguka na kumaliza wa mwisho kwenye mbio hizo.

Mkenya mwingine Edinah Jebitok hakufuzu kwenye fainali baada ya kumaliza katika nafasi ya kumi na mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here