Watu 144 wamekutwa na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 2,917 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 103,332.
Katika taarifa waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu 55 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 85,391.
Watu 4 zaidi wameaga na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,801.
Wagonjwa 267 wamelazwa katika hospitali wengine 1,187 wanashughulikiwa nyumbani.
Idadi ya watu walio katika hali mahututi ni 20.
Msambao katika kaunti ni kama ifuatavyo Nairobi 73, Busia 17, Mombasa 14, Kiambu 8.