Kenya yaripoti maambukizi mapya 431 ya corona

0

Mtoto wa miezi minne na ajuza mwenye umri wa miaka tisini ni miongoni mwa watu 431 waliopatwa na ugonjwa wa corona kati ya sampuli 5,846 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 169,356 huku kiwango cha maambukizi nchini kikiwa asilimia 7.4%.

Katika muda huo, watu 31 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 115,844 huku 10 zaidi wakifariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 3,097.

Takwimu za wizara ya afya zinaonesha kuwa idadi ya waliopata chanjo dhidi ya ugonjwa huo imefikia 960,379.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here