Kenya yanyakua medali kwenye mjini Tokyo Japan

0

Wanariadha wa Kenya wameshinda medali mbili kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea mjini Tokyo, Japan.

Mwanariadha Benjamin Kigen ameshinda medali ya kwanza kwa kunyakua SHABA baada ya kumaliza wa tatu kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Kwa mara ya kwanza, mwanariadha Soufiane El Bakkali wa Morocco ameshinda dhahabu kwenye mbio hizo ambazo kwa miaka 37 zimekuwa zikitawaliwa na Wakenya.

Muithopia Lamecha Girma amenyakua nishani ya FEDHA baada ya kumaliza wa pili kwenye mbio hizo.

Hellen Obiri aliishindia Kenya nishani ya pili baada ya kumaliza wa pili na kushinda FEDHA kwenye mbio za mita 5,000 kwa wanawake.

Sifan Hassan wa Uholanzi alishinda dhahabu huku Muithopia Gudaf Tsegay akishinda SHABA baada ya kumaliza wa tatu kwenye mbio hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here