Kenya na Tanzania wameahidi kuboresha ushirikiano wa karibu baina yao ili kuwa na uhusiano wa kudumu kwa manufaa ya raia wake.
Ndio makubaliano yaliyoafikiwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza rasmi ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
Mazungumzo hayo yameangazia namna ya kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na Tanzania kibiashara ikiwemo kuondoa vikwazo kwenye mipaka yake.
Wawili hao aidha wametia saini mkataba wa makubaliano kujenga bomba la gesi kutoka Mombasa hadi Tanzania ili kuwawezesha raia wake kupata umeme kwa urahisi.