Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja ameachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kupatikana na hatia ya kudharau amri ya mahakama kufuatia kufungwa kwa baadhi ya barabara jijini Nairobi wakati wa maandamano ya Juni 25, 2026.
Jaji Patricia Nyaundi amesema hakuna haja ya kumpa Kanja adhabu kali kwa tukio hilo, lakini ameonya kuwa mahakama haitasita kutoa adhabu kali zaidi iwapo ukiukaji wa amri za mahakama utajirudia.
“Hakuna haja wala manufaa ya kumpa Kanja adhabu kwa tukio la sasa, lakini mahakama haitasita kutoa adhabu kali zaidi iwapo mwenendo huo utajirudia,” amesema Jaji Nyaundi.
Jaji Nyaundi pia amezingatia hatua ya Kanja kufika mwenyewe mbele ya mahakama akiwa ameandamana na maafisa wakuu wa polisi, pamoja na ahadi yake ya kuhakikisha amri za mahakama zinawafikia maafisa walio chini ya uongozi wake.
Kanja alipatikana na hatia baada ya polisi kuweka vizuizi barabarani katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi mnamo Juni 25, bila kutoa taarifa kwa umma kama ilivyohitajika chini ya amri ya awali ya mahakama.
Kesi hiyo ilitokana na amri ya muda iliyotolewa Julai 2025, iliyokuwa ikiitaka Huduma ya Kitaifa ya Polisi kuwafahamisha wananchi kabla ya kuweka vizuizi vya dharura barabarani.
Shirika la Katiba iliwasilisha kesi hiyo baada ya polisi kuzuia umma kuingia jijini









