KAMPUNI YA CROWN BUS INATUMIWA KUFADHILI ALSHABAAB MAREKANI YASEMA

0

Marekani imewawekea vikwazo wakenya wawili na kampuni moja ya mabasi baada ya kuhusishwa na utakatishaji wa fedha kwa minajili ya ufadhili wa kundi la kigaidi la Alshabaab.

Kupitia tangazo kwa vyombo vya habari marekani imesema kampuni ya mabasi ya masafa marefu ya Crown bus imekuwa ikitumiwa na Faysal Yusuf Dini na Mohamed Jumale Ali Awale kuwezesha usafiri wa fedha na rasilimali nyingine kwa Alshabaab.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Marekani Mathew Miller amesema kampuni na watu waliowekewa vikwazo ni mtandao wa kimataifa wenye shughuli katika upembe wa afrika, Uarabu na taifa la Cyprus.

“Tishio linaloletwa na al-Shabaab si la Somalia pekee. Mapato ya Al-Shabaab yanatolewa kwa makundi mengine yenye uhusiano na al-Qa’ida duniani kote na kusaidia kufadhili malengo ya al-Qaida duniani kufanya vitendo vya kigaidi na kudhoofisha utawala bora.” Miller amesema.

Watu na mashirika mengine yaliyo kwenye orodha hio ya vikwazo ni pamoja na Haleel Group yenye makao yake Dubai na matawi nchini Kenya na Uganda, Hassan Abdirahman miongoni mwa wengine.

Kutokana na hilo mali inayomilikiwa na watu waliokwenye orodha hio na kampuni waliona hisa zaidi ya asilimia hamsini ndani ya marekani itafungiwa.

“Raia wa Marekani aidha wanaonywa dhidi ya kufanya biashara moja kwa moja au kupitia mawakala na waliorodheshwa’’ taarifa hio imeongeza.

Marekani imekuwa mshirika mkuu wa vita dhidi ya kundi la Alshabaab ambalo limetekeleza mamia ya mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Upembe wa AFrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here