Awamu ya kwanza ya kampeini ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio wa kaunti 13 imekamilika huku watoto milioni 3.4 walio chini ya miaka mitano wakilengwa.
Awamu ya pili inatazamiwa kuanza Juni 19 na kuendelea hadi Juni 23 mwaka huu.
Akihutubia wanahabari kutoka mtaani Kibra alipokuwa anakagua namna shughuli hiyo inaendelea, Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hadi kufikia Jumanne, watoto milioni 2.5 wamechanjwa dhidi ya Polio tangu kampeni hiyo kuanza Jumamosi iliyopita.
Waziri Kagwe amesema visa sita vya Polio yenye mfumojeni wa Somalia vimeripotiwa nchini mwaka huu, huku akiwahimiza wazazi na walezi kuzingatia usafi na kuhakikisha kuwa wanao wanachanjwa
Visa sita vya ugonjwa wa polio vilripotiwa kaunti ya Garrisa na Mombasa, hali iliyoletaa wasi wasi wa kuwepo mkurupuko wa virusi vya polio nchini.