Mamlaka ya kumulika utendakazi wa Polisi (IPOA) imeanzisha uchunguzi kufuatia mauji yanayodaiwa kutekelezwa na Polisi wakati wa maandamano mtaani Kahawa West.
Mwenyekiti wa IPOA Anne Makori kupitia taarifa anasema tayari wametuma kikosi chake katika eneo hilo kuchunguza lengo likiwa ni kubaini kilichojiri na kupendekeza hatua zitakazofuata.
Wakaazi wanadaiwa kuwa watu wawili walipigwa risasi wakati wa maandamano ya kupinga ubomozi wa vibanda uliofanywa na shirika la NMS.
OCPD wa Kasarani Peter Mwanzo licha ya kutodhibitisha taarifa za mauaji amewatetea maafisa wake akisema waandamanaji hao waliwadhubutu kuwashambulia Polisi waliotumwa kupambana na ghasia.
Waandamanaji wanaopinga ubomozi wa vibanda vyao walibeba mwili wa mmoja wa wawili hao wakidai walipigwa risasi na maafisa hao wakati wakipigania haki yao.