Huenda mashindano ya Olimpiki Tokyo yakahairishwa tena

0

Mkuu wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya Olimpiki mjini Tokyo, Japan hajafutilia mbali uwekezano wa kusitisha mashindano hayo kunako dakika za mwisho iwapo maambukizi ya ugonjwa wa corona yatapindukia.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kuulizwa swali hilo, Toshiro Muto amesema wanafuatilia kwa karibu msambao wa virusi hivyo na atakuwa tayari kufanya mashauriano na waandalizi wa mashindano hayo yatakayoanza Ijumaa hii iwapo hilo litalazimu.

Kuongezeka kwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo kulisababisha kuhairishwa kwa mashindano hayo mwaka jana huku waandalizi wake wakisema yafanyika mwaka huu bila mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here