“Hatutasalimu Amri kwa Matamshi ya Kisiasa” Joho Aeleza Kwa Nini Leseni ya Tata Ilifutwa.

0
Waziri wa Madini Ali Hassan Joho.
Waziri wa Madini Ali Hassan Joho.

Waziri wa Madini, Hassan Ali Joho, amefafanua kwa nini hasa serikali ilifuta leseni ya Kampuni ya Tata

Joho amesema Serikali ilifuta leseni hiyo baada ya kampuni hiyo kushindwa kutimiza masharti iliyowekewa kufuatia notisi iliyotolewa mwezi Julai.

“Mnamo mwezi Julai, tulitoa notisi ya uzingatiaji wa masharti. Hii ina maana kwamba ulikuwa umevunja masharti haya, na tulitarajia uyatekeleze.” Amesema Joho.

Aidha amesema miongoni mwa masharti hayo ni kulipa fidia kwa jamii zilizoathiriwa na shughuli za uchimbaji katika ardhi yao, pamoja na kusitisha usafirishaji wa malighafi nje ya nchi bila kuongezwa thamani hapa nchini.

“Unapoenda kuomba leseni ya madini, unaainisha wazi namna utakavyowasaidia wananchi wa eneo hilo. Ikiwa hilo halijatekelezwa, unafikiri nitasalimu amri kwa matamshi ya kisiasa?” Amehoji Joho.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, Serikali haikuona dalili za kutosha zinazoashiria kuwa kampuni hiyo ingetekeleza masharti yote kikamilifu ndani ya muda uliowekwa.

Hatua hiyo, amesema Joho, ililazimu Serikali kuchukua uamuzi wa kuifuta leseni ya Tata.

Waziri Joho pia amekanusha madai ya upinzani kwamba kufutwa kwa leseni ya Tata ni sehemu ya njama ya kuiondoa kampuni hiyo ili kupisha kampuni nyingine, ambayo inadaiwa kuwanufaisha baadhi ya watu serikalini.

Joho amesema uamuzi huo ulitokana na kutotekelezwa kwa masharti yaliyowekwa na Serikali, akisisitiza kuwa hatua hiyo haikuchochewa na maslahi binafsi au kisiasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here