“HATUKUNYANG’ANYI CHEO” OBURU AMWAMBIA NAIBU RAIS KINDIKI

0
Oburu Oginga

 

Siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 zimeendelea kupamba moto baada ya kujitokeza waziwazi katika hafla ya kuwawezesha vijana kupitia mpango wa Nyota, iliyofanyika jijini Kisumu.

Hafla hiyo iliongozwa na Rais William Ruto na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa chama cha ODM, akiwemo kiongozi wa chama hicho Oburu Oginga.

Oburu katika hafla hiyo ambayo ilifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta huko Kisumu, Oburu amesadiki kwamba Chungwa linalenga mazungumzo na UDA kabla ya uchaguzi ujao.

“Mazungumzo yanaposhika kasi, Naibu Rais usidhanie tunataka cheo chako yakwamba tunataka kukufukuza. Wewe ni Rafiki yetu.’’ Alisema Oburu

Hata hivyo Oburu ametaja kwamba ODM sio chama cha kabila moja na hivyo kinalenga kujumuisha kila mmoja.

“Katika meza ya mazungumzo, tutakuwa tunalenga kupata kile ambacho ODM inafaa kupata’’, aliongeza Oburu.

Aidha, kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kusisitiza kuunga mkono uongozi wa Rais William Ruto Pamoja na miradi ambayo anaendeleza huku akiwasuta wanaodharau ODM kuungana na UDA.

“Uchaguzi ni mwaka ujao na lazima tujipange mapema. Ninawahakikishia nitawapeleka Canaan na tutapitia Singapore”, Oburu ameongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here