Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amepatwa na virusi vya corona.
Naibu Gavana Titus Ntuchiu amedhibitisha kuwa gavana huyo amejitenga kulingana na taratibu za wizara ya afya.
Waziri wa afya katika kaunti hiyo Misheck Mutuma amesema kuwa kaunti ya Meru kwa sasa ina visa 137 vya corona vilivyodhibitishwa kufikia sasa.
Mutuma amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kuendelea kuzingatia masharti ya usalama kuzuia msambao wa visa hivyo.