GAVANA WA KERICHO ERIC MUTAI ANAITAKA SERIKALI YA KAUNTI KUVUNJWA

0

Gavana wa kaunti ya Kericho Eric Mutai amesema kuwa yuko tayari kuongoza mchakato wa kukusanya saini za wakazi wa kaunti hiyo ili serikali nzima ya kaunti ivunjiliwe mbali na uchaguzi kufanywa upya

Akizungumza saa chache baada ya mswada wa kumbandua ofisini kuwasilishwa katikabunge la kaunti hiyo na mwakilishi wadi wa Sigowett Kiprotich Rogonyi Gavana Mutai amesema mpango huo wa kubanduliwa ni njama ya baadhi ya wanasiasa wa kaunti hiyo wanaokilenga kiti chake hali ambayo imechangia kulemazwa kwa miradi mingi ya maendeleo katika kaunti hiyo

Aidha Gavana Mutai anayekabiliwa na shutma za ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi miongoni mwa mengine anajutia kumetua Fred Kirui kuwa naibu wake kwani ni miongoni wa wanaoshinikiza ajenda ya kubanduliwa kwake

Hata hivyo ameahidi kuwa yu tayari kujiwasilisha kwenye mabunge yote mawili ya kaunti na lile la seneti kujibu madai yanayomkabili

Ikumbukwe mara ya kwanza aliokolewa na seneti baada ya bunge hilo kusema kwamba sheria haikuzingatiwa katika mchakato wa kumbandua

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here