Maafisa wa polisi wamewakamata washukiwa wawili wa ulanguzi wa pembe za ndovu wakiwa na pembe za dhamani ya shilingi milioni 1.8 kwenye kaunti ya Migori
Washukiwa hao wamekamatwa kwenye oparesheni ya pamoja iliyofanywa na maafisa wa poisi kwa ushirikiano na wale wa shirika za hudma ya wanyamapori KWS
Wawili hao wamekamatwa kwenye eneo la Namba kaunti ya Migori huku polisi wakinasa pikipiki zilizokuwa zikisafirisha pembe hizo za uzani wa kilo 18.8
Waliokamatwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35 na mwanamme mwenye umri wa miaka 58 huku wakiendelea kuzuiliwa wakisubiri kuwasilishwa mahakamani









