Gavana wa kaunti ya Kitui Charity Ngilu amelezwa katika hospitali ya Nairobi baada ya kupatwa na ugonjwa wa corona.
Haya yamefichuliwa na mwenzake wa Machakos Dkt. Alfred Mutua ambaye ameomba Wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya usalama.
Dr. Mutua amesema haya kwenye hafla ya wasanii katika kaunti ya Murang’a na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.









