Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imejitenga na sintofahamu inayozingira kutumwa kwa nakala tofuati za mswada wa marekebisho ya katiba BBI kwenye mabunge ya kaunti.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati katika taarifa amejitetea akisema walituma nakala asili walizopewa naq wendani wa BBI.
Watalaamu walioajiriwa na bunge kutathmini nakala za mswada huo wanadai kuwa mabunge 13 pekee ya kaunti ndiyo yalijadili na kupitisha mswada sahihi wa BBI.
Baadhi ya nakala za mswada huo zimegunduliwa kuwa na vipengee tofauti vya katiba na hivyo kufanya vigumu kwa bunge kuamua hatma ya mswada huo.
Ikumbukwe kwamba mswada huo ulipitishwa na mabunge ya kaunti yapatayo 43 na hivyo kutoa nafasi ya kuandaliwa kwa mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia kura ya maamuzi.