Bunge la Senate limepiga kura ya kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI.
Maseneta hamsini na mbili (52) walipiga kura ya NDIO huku maseneta kumi na mbili (12) wakipiga kura ya LA.
Wendani wa naibu Rais William Ruto wakiongozwa na maseneta Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet), Irungu Kang’ata (Murang’a) na Susan Kihika (Nakuru) walipiga LA kupinga mswada huo kwenye kikao kilichokumbwa na malumbano.
Kiongozi wa wachache katika bunge hilo James Orengo na Seneta wa Baringo Gideon Moi wameongoza maseneta wengine kupiga kura ya NDIO kwa mswada huo.
Tayari bunge la kitaifa limepitisha mswada huo baada ya spika Justin Muturi kuzima juhudi za kuufanyia mabadiliko mswada huo.









