Atwoli aunga mkono kubaniwa kwa picha na video za utupu

0

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini (COTU) umeunga mkono mswada unaotaka kupigwa marufuku kwa uchapishaji na usambazaji wa picha na video za utupu.

Mswada huo wake mbunge wa Garissa Mjini unapendekeza faini ya Shilingi Milioni 20 au kifungo cha miaka 25 jela kwa watakaopatikana wakichapisha au kutuma video na picha za ngono.

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli anasema kuharamishwa kwa tabia hiyo kutawezesha maadili mema kazini kwa sababu baadhi ya watu wamekosa kuwa na mienendo inayofaa kwa sababu wanatizama picha na video za utupu hata wakiwa kazini.

Kwa kuzingatia hayo yote, Atwoli amewahimza wabunge wote kuunga mkono mswada huo wa Daule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here