Aliyekuwa wakili wa naibu rais William Ruto, Karim Khan ameapishwa rasmi kuwa mwendesha mkuu wa mashtaka wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC.
Wakili huyo kutoka Uingereza anachukua majukumu kutoka kwa mtangulizi wake kutoka Ghana Fatou Bensouda kwa kipindi cha miaka tisa.
Akizungumza wakati wa uapisho wake, Karim Khan amesema jukumu lake la kwanza ni kukomesha tabia ya watu kufanya makosa pasipo kuheshimu sheria.
Wakili huyo,51, ana uzoefu wa miaka nyingi katika mahakama za kimataifa kama mwendesha wa mashtaka, mchunguzi na mwanasheria.