Aliyekuwa Kamishna wa IEBC Afariki Dunia.

0

Aliyekuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) Mohamed Abdullahi Sharawe ameaga dunia.

Kuliingana na Familia yake Sharawe alifariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Aliwahai kuwa Katibu Mkuu wa Idara ya Barabara na Kazi za Umma wakati wa utawala wa Hayati Rais Daniel Arap Moi kabla ya kuhudumu katika Wizara ya Utafiti, Mafunzo ya Ufundi na Teknolojia, akichangia katika uundaji wa sera kuhusu elimu ya ufundi, utafiti na teknolojia inayotumika.

Mnamo mwaka 2009, Sharawe aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Marehemu Rais Mwai Kibaki kuhusu Masuala ya Waislamu na baadaye kuwa Kamishna wa Tume ya Mpito ya Mapitio ya mpaka maarufu Ligale Commission.

Baada ya kutangazwa kwa Katiba yam waka 2010 Sharawe aliteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa kwanza wa IEBC alikohudumu kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2016.

Katika kipindi hicho alisimamia uchaguzi mkuu wa 2013 uliokuwa wa kwanza chini ya Katiba mpya.

Aidha aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa umma akihamasisha uwajibikaji, uadilifu na taaluma katika Utumishi wa umma.

Viongozi mbalimbali wamemtaja Sharawe kuwa mfano wa uongozi bora, uzalendo na huduma kwa taifa huku wakituma risala za rambirambi kwa familia, marafiki Pamoja na jamaa wake.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here