Abdulkadir Haji aapishwa rasmi kuwa seneta wa Garissa

0

Abdulkadir Haji ameapishwa rasmi kuwa Seneta wa kaunti ya Garissa kwenye kikao maalum cha bunge la Senate kilichoitishwa na spika Ken Lusaka.

Haji alichaguliwa pasipo kuandaliwa kwa uchaguzi baada ya kukosekana kwa yeyote wa kumpinga.

Maseneta akiwemo George Khaniri (Vihiga) na Kimani Wamatangi (Kiambu) wamempongeza Abdulkadir na kumtakia kila la heri anapofuata nyayo za babake marehemu Yusuf Haji katika kutekeleza majukumu yake.

Tume ya uchaguzi IEBC ilichampisha jina la Haji kuwa seneta wa Garissa kumrithi babake aliyefariki Feberuari 15 mwaka huu.

Kikao hicho maalum vile vile kinaangazia mswada wa ugavi wa mapato uliowasilishwa kutoka kwa bunge la kitaifa juma lililopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here