Kenya yaripoti maambukizi mapya 241 ya corona, 20 wafariki

0

Watu 241 wamekutwa na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 2,515 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 151,894

Katika taarifa, Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu 636 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 102,278 huku maafa 20 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,501.

Kuhusu shughuli ya utoaji chanjo ya Astrazeneca inayoendelea kote nchini, waziri Kagwe ametangaza kuwa jumla ya watu 702,170  wamepata chanjo hiyo ikiwemo watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi 397,539, wahudumu wa afya 141,146, maafisa wa usalama 57,338, walimu 106,147

Miongoni mwa waliochanjwa ni wanaume 393,261 na wanawake 308,526.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here