WATU 649 WAAFA KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI

0

Takriban watu 649 wameaga dunia kutokana na ajali za barabarani tangia mwaka huu ulipoanza.

Kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka ya usafiri barabarani (NTSA), hii inaashiria ongezeko la maafa kwa asilimia 4.2 ikilinganishwa na mwaka jana.

NTSA imedokeza katika kipindi cha hadi tarehe 20 mwezi huu wa Februari, watu 252 waliokuwa wakitembea kwa miguu wameaga dunia kutokana na ajali ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana ya watu 190.

Takwimu za NTSA pia zimebainisha madereva 43 wamepoteza maisha pamoja na waendesha bodaboda wafikiao 158.

Vilevile abiria 125 na waendesha baiskeli 10 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani katika kipindi hicho cha kuanzia tarehe Mosi mwezi Januari mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here