Wakosoaji wa BBI watetea uamuzi wa kusitisha mchakato huo

0

Rais Uhuru Kenyatta alifaa kuachia majukumu yake kama kiongozi wa taifa alivyofanya wakati wa kesi za ICC ili kusukuma mabadiliko ya katiba kupitia mchakato wa BBI.

Ni baadhi ya hoja za wanaunga mkono uamuzi wa mahakama kuu uliosimamisha marekebisho hayo ya katiba.

Profesa Kindiki Kithure akiwasilisha hoja zake mbele ya jopo la majaji saba wa mahakama ya rufaa amesema rais alitumia visivyo mamlaka yake kupigia debe mchakato huo huku akitumia pesa za umma kuendelea ajenda hiyo ya kubadilisha katiba.

Wakili Nelson Havi ambaye amewakilisha wanaopinga mchakato huo akiwemo mwanauchumi David Ndii amewaambia majaji hao kwamba katiba ya sasa hairuhusu mtu yeyote kuhitilafiana na uhuru wa mihimili tatu ya serikali ambayo ni Bunge, Mahakama na Afisi ya Rais.

Kwa upande wake wakili Esther Ngawa ameshikilia msimamo kuwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC haikuwa imebuniwa ipasavyo wakati iliidhinisha saini za mswada wa BBI.

Ngawa ambaye pia anawakialisha wanaopinga mchakato huo anasema jaji wa mahakama kuu Chacha Mwita aliruhusu IEBC kuandaa chaguzi ndogo na makamishna watatu pekee kwani kuna sheria ya kuongoza zoezi hilo, kinyume na kura ya maamuzi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here