Mahakama kuu imebatilisha uteuzi wa Dorothy Jemator kuwa mwakilishi wa chama cha mawakili (LSK) kwenye jopo la kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya uchaguzi IEBC.
Badala yake jaji wa mahakama kuu George Odunga amemuagiza spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi kukabidhiwa jina la Morris Kimuli kuwa mwakilishi wa LSK kwenye jopo hilo.
Uhasama ndani ya LSK baina ya rais Nelson Havi na afisa mkuu mtendaji Mercy Wambua uliishia kwa kila mmoja kumteua anayetaka kuhudumu kwenye jopo hilo.
Havi alimteua Kimuli huku Wambua akimteua Jemator.
Makamishna wengine kwenye jopo hilo ni; mwenyekiti Dr Elizabeth Muli; Gideon Solonka; James Achoka Awori; Elizabeth Odundo Meyo; askofu Joseph Mutie na Dr Farudin Suleiman Abdalla.









