Kilichosababisha kifo cha Wycliffe Omwenga, shahidi mkuu kwenye kesi ya mauaji ya nduguye na mfanyibiashara Kelvin Omwenga hakijagunduliwa mara moja.
Hii ni baada ya matokeo ya upusuaji kukosa kuweka bayana chanzo halisi cha kifo chake.
Familia ya marehemu imetakiwa kusubiri ripoti ya sumu itakayotoa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha kifo hicho.
Familia hiyo imeondoka kwenye hifadhi ya maiti bila majibu kuhusu kilichomuua Wycliffe.
Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya Nairobi Women na mpasuaji wa serikali Charles Muturi na kuhudhuriwa na Polisi.
Wycliffe alikuwa shahidi muhimu kwenye kesi ambapo Chris Obure na mlinzi Robert Ouko wameshtakiwa kwa mauji.