Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya kuapishwa rasmi kwa majaji 34 katika Ikulu ya rais Nairobi licha ya utata kuzingira kukataliwa kwa majaji wengine SITA walioteuliwa na tume ya huduma za mahakama JSC.
Majaji hao waliokula kiapo kulinda katiba ni majaji wa mahakama ya Rufaa, mahakama ya Leba pamoja na mahakama ya Mazingira.
Uapisho huo umefanyika licha ya Katiba Institute kuwasilisha kesi mahakamani kuzuia shughuli hiyo hadi majaji sita ambao rais Kenyatta alikataa kuwaidhinisha watakapoteuliwa rasmi.
Sita hao waliosalia ni pamoja na Weldon Korir, Aggrey Muchelule, George Odunga na Joel Ngugi pamoja na Evans Makori na Judith Omange.