Mahakama ya Migogoro ya vyama vya kisiasa imeruhusu vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Senet awa Nairobi Edwin Sifuna kuhifadhi jina The Mwananchi Party wakati ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa kuhusu mzozo wa usajili wa jina hilo
Mahakama hiyo pia imeruhusu kuhifadhi na kusajili jina Liberty National Democratic Alliance linalojulikana kwa ufupi kama LINDA hadi pale rufaa hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa
Katika maagizo ya mda yaliyotolewa kupitia kikao cha mtandaoni PPDT imemzuia msajili wa vyama vya kisiasa kuzingatia, kuhifadhi au kusajili jina Linda Mwananchi au jina Lolote linalofanana na hilo kwa mtu au taasisi nyingine yeyote
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa tarehe 14 Septemba 2026
Akizungumza jijini Nairobi kiongozi wa Linda Mwananchi Edwin Sifuna amesema wanachokipigania sio chama kipya bali kulinda jina na utambulisho wa kisiasa wanaodai kuwa ni wao
“Tunachopigania si chama cha kisiasa, kwa sababu tayari tuna vyama; tunachopigania ni chapa yetu na jina letu.” Alisema Sifuna
Sifuna amesema walimpeleka msajili wa vyama vya kisiasa mahakamani kwa kuwa hawaoni sababu ya kunyimwa jina hilo
Kwa upande mwingine viongozi wa chama cha LINDA wakiongozwa na kiongozi wao Phanesio Thuku, wameendelea kusisitiza kuwa LINDA ni jina lao halali
“Hatutamruhusu mtu yeyote kutumia utambulisho wetu,” alisema kiongozi wa chama cha LINDA, Phanesio Thuku.
“Chama cha LINDA kilisajiliwa mwezi Novemba 2024 na kina wanachama kote nchini, ingawa bado hakijapokea cheti rasmi cha usajili kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa.” Aliongeza Thuku









