Kenya hii leo imejiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku.
Lengo kuu la maadhimisho haya ni wito kwa waraibu wa bidhaa za tumbaku kuacha kuzitumia kutokana na madhara yake kwa mwili.
Mwenyekiti wa shirika la kudhibiti matumizi ya tumbaku nchini (KETCA) Joel Gitali anasema watu elfu 30 hufa kila mwaka humu nchini kutokana na uvutaji wa sigara.
Mmoja wa watu walioacha uvutaji wa sigara ni John Rugunya ambaye anaeleza kuwa uamuzi huo haukuwa rahisi kutekeleza hadi pale alipogundua jambo lisilo la kawaida lililomuwacha kinywa wazi.