Si haki ya polisi kuchukua hongo – Mutyambai

0

Huku ikiripotiwa kwamba Polisi wanachukua hongo ya kati ya Sh50 na Sh100 kutoka kwa matatu zinazokiuka masharti ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai anawarai wananchi kuripoti visa kama hivyo.

Akijibu maswala ya wananchi kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter, Mutyambai amesema Polisi hawaruhusiwi kuitisha wala kupokea hongo na kwamba visa kama hivyo vinastahili kuripotiwa katika kituo cha polisi kilicho karibu.

Kuhusu madai ya matatu kubeba abiria kama kawaida kinyume na inavyohitajika, Mutyambai amesema linasalia jukumu la kila mmoja kushirikiana ili kuhakikisha kwamba msambao wa virusi vya corona umepungua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here