Rais wa chama cha mawakili nchini LSK Nelson Havi amekamatwa kufuatia tuhuma za kumjeruhi afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo Mercy Wambua.
Naibu Rais wa LSK Carolyne Kamende amesema Havi ameshikwa na kupelekwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi nchini DCI kuhojiwa.
Havi anakamatwa siku moja baada ya Wambua kuandikisha ripoti katika kituo cha polisi cha Muthangari akidai kuwa Havi alimdhulumu wakati wa mkutano katika afisi zao, barabara ya Gitanga kaunti ya Nairobi.
Hata hivyo Havi tayari amekanusha madai ya kumuumiza Wambua na badala yake kumtuhumu kwa kujitoma bila ruhusa ndani ya chumba cha mkutano ilhali mkutano ulikuwa ukiendelea.