Rais wa Tanzania Samia Suluhu atawasili humu nchini hapo kesho kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Atakapowasili nchini, Rais Samia atapokelewa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta kabla ya wawili hao kufanya mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili.
Uhusiano wa Kenya na Tanzania ulikumbwa na changamoto si haba wakati wa utawala wa hayati John Magufuli haswa kutokana na mbinu tofauti zilizotumika na mataifa haya kukabili janga la covid19.
Kwa sasa, Rais Samia amebuni jopo la wataalam kumshauri kuhusu mbinu za kupambana na janga hilo nchini Tanzania.
Mazungumzo baina ya wawili hao pia yatajikita katika kuimarisha biashara baina ya mataifa hayo huku Rais Samia akiratibiwa kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyibiashara wa Kenya na Tanzania.
Rais Samia ameratibiwa pia atahutubia kikao cha pamoja cha bunge la kitaifa na seneti.