Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai wameahidi kuwaadhibu maafisa wa Polisi wanaodaiwa kuwapiga risasi watu wawili katika kituo cha Polisi cha Rioma kaunti ya Kisii.
Matiang’i na Mutyambai wametembelea eneo hilo kutathmini hali kufuatia maandamano ya juma lililopita kulalamikia mauaji hayo.
Akikashifu mauaji hayo, gavana wa Kisii James Ongwae ameomba kuwepo kwa utulivu huku uchunguzi ukiendelea.