Polisi kuchunguza mauaji ya ndugu wawili Embu

0

Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai ameagiza kuanzishwa kwa uchunguzi kufuatia mauaji ya ndugu wawili waliofariki baada ya kushikwa na Polisi Embu.

Mutyambai ametaka uchunguzi huo kubaini ni vipi ndugu hao Benson Njiru na Emmanuel Mutura wanaodaiwa kushikwa Jumapili kwa kuvunja masharti ya kafyuu walifariki.

Wakatu uo huo mamlaka ya kumulika utendakazi wa Polisi (IPOA) imewatuma wachunguzi wake Embu kuchunguza mauaji hayo.

IPOA inasema baada ya uchunguzi, itapendekeza wahusika kufunguliwa mashtaka ya mauaji iwapo utepetevu wa maafisa wa polisi waliowakamata ulichangia vifo cha wawili hao.

Mkuu wa Polisi Embu Mashariki Emily Ngaruiya amewatetea maafisa wake akisema ndugu hao walikufa baada ya kuruka kutoka kwa gari la Polisi baada ya kukamatwa kwa madai ya kuwa nje wakati wa kafyu.

Hata hivyo familia inasema wawili hao waliteswa na kisha kuuawa na maafisa wa Polisi baada ya kukamatwa katika eneo la Kianjokoma Jumapili usiku.

Familia hiyo inashangaa mbona maafisa hao hawakupiga ripoti wakati kisa hicho kilifanyika na kusubiri hadi wakati familia ilianza kutafuta wapendwa wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here