PEP yajiondoa Kiambaa kwa faida ya UDA

0

Chama cha Peoples Empowerment PEP kinachoongozwa na mbunge wa Gatundu Kusii Moses Kuria kimejiondoa kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi mdogo eneobunge la Kiambaa.

Katika taarifa, Kuria amesema amechukua ahtua hiyo ili kudumisha umoja katika vuguvugu la mahasla, baada ya kushauriana na naibu Rais William Ruto.

Hatua ya PEP kuwa na mgombea katika uchaguzi huo mdogo ilipingwa na wabunge Rigathi Gachagua wa Mathira na Kimani Ichungwa wa Kikuyu ambao badala yake wanapendelea muwaniaji wa chama cha United Democratic Alliance UDA kinachohusishwa na Dr Ruto.

Tayari chama cha UDA kimemteua John Njuguna kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi huo huku Jubilee imemteua Kariri Njama.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa sehemu hiyo Paul Koinange.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here