Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji amesema azimio lao ni kuhakikisha kwamba wameimarisha utendakazi wao kwa manufaa ya mwananchi.
Aizungumza alipozindua tararibu za utendakazi bora kwa afisi hiyo, Hajji amesema kupitia kuimarisha utendakazi wao, taifa litafaulu katika kupambana vilivyo na uhalifu.
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi alikuwepo wakati wa uzinduzi huo amesema hatua hiyo itapiga jeki vita dhidi ya uhalifu kupitia kushtakiwa kwa wahalifu baada ya uchunguzi wenye umakini.