Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amekashifu vikali matumizi mabaya ya polisi katika maeneobunge ya Bonchari na Juja wakati wa chaguzindogo zilizofanyika jana.
Katika taarifa, Odinga ametaja visa vya unyanyasaji wa vilivyotekeleza na maafisa hao kama kiburi na kutokujali kwa baadhi ya maafisa wabinafsi wa serikali.
Waziri huyo mkuu wa zamani anasema maafisa hao wa serikali wenye kiburi wanataka kuleta kwa handisheki baina yake na Rais Uhuru Kenyatta na kurudisha nyuma hatua zilizopigwa hadi kufikia sasa.
Odinga anasema amani iiliyoshuhudiwa nchini kufuatia mkataba wao haifai kuchukuliwa kwa kawaida.
Maafisa wa usalama walidaiwa kuvunja mikutano ya kampeni ya wanasiasa wa vyama vya ODM na UDA kando na kuwakamata baadhi ya viongozi na maafisa wa vyama hivyo na kuwazuiliwa kinyume cha katiba.