Naibu Gavana wa Wajir Ahmed Muktar kuapishwa leo kuwa Gavana

0

Naibu Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Ali Muktar anatazamiwa kuapishwa wakati wowote kuanzia sasa kumrithi aliyekuwa Gavana Mohamed Abdi Mohamud aliyetimuliwa.

Hafla ya kuapishwa kwa Muktar inafanyika katika makao makuu ya serikali ya kaunti hiyo na inaongozwa na kamati ya mpito, siku moja tu baada ya maseneta kuidhinisha hoja ya kumbandua afisini.

Baadhi ya wakaazi wa kaunti hiyo wamekaribisha kutimuliwa kwa Abdi na kuelezea imani yao kuwa uongozi mpya utatataua shida zao.

Maseneta 25 walipiga kura ya kuunga mkono kungolewa afisini kwa Gavana huyo huku maseneta wawili wakipinga na wengine wanne kutopiga kura.

Abdi sasa ni Gavana wa tatu kungolewa afisini baada ya Mike Sonko wa Nairobi na Ferdinand Waititu wa Kiambu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here