Maafisa wa polisi wanamzuilia mwanamke mmoja kuhusiana na mauaji ya mwanaume mwenye umri wa miaka 35 katika eneo la Kwambuzi-Kiboko, Tigoni kaunti ya Kiambu.
Mshukiwa Grace Nyambura Njeri anatuhumiwa kumuua mwanaume huyo kwa kumdunga kisu kifuani mara kadhaa.
Mshukiwa anatazamiwa kufikishwa mahakamani leo kufunguliwa mashtaka.
Wakati uo huo, maafisa wa idara ya upelelezi nchini DCI wanachunguza mauaji ya mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 32 katika eneo hilo la Tigoni.
Mwili wa Duncan Kavucho Lugulu ulipatikana kando ya barabara ukiwa na majeraha ya visu.